Tuesday, September 19, 2017

Namna ya Kufanikiwa katika Biashara zako

Jifunze namna ya kufanikiwa katika biashara zako
Awali ya yote napenda kuwapa salamu zangu ndugu wajasiriamali wote ambao kwa ujumla mnahitaji mafanikio makubwa katika mipango yenu hali kadhalika na maisha kwa ujumla. Katika hali ya kawaida kila mmoja wetu angependa kuona mipango yake ikifanikiwa na kuwa imara kabisa. kufanikiwa  huko ndio njia pekee ya kubadili maisha yako na kuwa miongoni mwa wafanyabiashara wakubwa duniani. ndoto zote hizi za mafanikio huja kwa wale ambao tayari wanataka kubadili mitazamo yao na kuwa chanya badala ya mitazamo hasi. mambo yafuatayo hapo chini yanaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa katika mafanikio ya biashara zetu:-


  •  MUDA; Muda ndio kitu cha muhimu zaidi katika mafanikio ya kila mmoja. Biashara yoyote inahitaji uzingatiaji wa muda kama vile muda wa kufungua biashara yako na muda ambao unapaswa kukaa katika biashara yako. wateja wengi wanahitaji kuwa na uhakika na muda ambao biashara yako inakuwa imeanza na kuisha ili kuweza kujenga mazoea na uaminifu katika biashara yako.  Kwa wale wenye biashara za msimu kama biashara za matunda au mazao pia wanahitaji kuzingatia muda kutonana na upatikanaji wa bidhaa zao uli kuteka soko na kupunguza hasara ya kuharibikiwa na bidhaa zao. (kuendana na Muda)
  •  


Saturday, January 21, 2017

JIFUNZE: NAMNA YA KUWA JASIRI/ SHUJAA

Ujasiri ni nini?

Ujasiri ni hali ya kuamua kufanya jambo gumu linaloweza kuwa si rahisi moyo wako au mtu mwingine kuamua kulifanya bali ukajitoa na kulifanya. mfano mtu unaweza kujitoa hata uhai wako ili hali uokoe watu wengine, ukafirisika hata mali zako ilihali uokoe maskini, ukajitosa mahali poote pale bila woga ili hali upate utakacho.

Ujasiri  haupo kwa kila mtu, wapo watu waoga hawawezi hata kujaribu jambo wao hutegemea tu watu wengine ndio maisha yao husonga mbele. Lakini wapo watu ambao hawajali maisha yao wanaweza kufanya lolote hatakama haliwezekani ilimradi waishi maisha mazuri au kupata vitu wavitakavyo kama vile mapenzi, pesa, utajiri n.k 

Ujasiri huja wenyewe pale moyo wako unapoamua jambo bilakipingamizi chochote.. hakuna mtu anayefundishwa ujasiri bali huja wenyewe kutokana na msukumo wa moyo au shinikizo la watu fulani au vitu fulani. "woga ni umaskini" ni kauli ambayo watu wanaojiamini na ni majasiri hutumia katika harakati za kimaisha... mfano unakuta mtu anapenda msichana fulani lakini hawezi kabisa hata kumtamkia anaishia tu kuumia sana na kujihisi kama hana bahati.kumbe ndio kukosa ujasiri kwenyewe.
Sababu za kukosa ujasiri
  1. kutojiamini; unakuta mtu anapenda sana vitu fulani au mtu fulani lakini kutokana na yeye kutojiamin anaweza kuvikosa au kumkosa mtu ampendae.......
  2. kujidharau, kuna baadhi ya watu ujiona wao si mali kitu.. wao wako hadhi ya chini kuliko wengine, au wakajihisi ni wabaya, weusi, waovu sana, hawana akili, maskini kuliko wengine hivyo kujidharau.
  3. Mitazamo hasi; hii ni mitadhamo iwayo akilini mwa watu ambapo mara nyingi watu hujiona kuwa sahihi kimazamo hasa upinzani wa vitu vyenye tija na kushikilia mitazao isiyo kuwa na tija... mfano kunawatu walisha amini kwamba hawawezi kitu kabisa ndio wakajidharau na kuishia kutojiamini.
  4. kukosa msaada/support; moyo wa mtu unaweza kukata tamaa na kutojiamini endapo kwa upande wake hakna anae msimamia wala kumtazama hata kama anafanya jambo la msingi badala yake wakajitokeza watu wanao mbeza au kumkejeli hivyo mtu akaona haina maana kuendelea na jambo alilolitarajia na kujikuta amepoteza ujasiri  n.k
Namna ya kuwa jasiri/ kuwa na ujasiri.
  • kujiamini; hakuna binadamu aliye kamilika, kama umeamua kufanya jambo lolote lenye msaada katika maisha yako au a wengine.. jiamini ujioe hata kama watu watakushangaa, au kukucheka, kukubeza kukukejeli n.k .... "uoga ni umaskini"
  • Simama imara mwenyewe; daima usitetereke kwa yale ambayo watu wanakunenea bali simama imara na sikuzote usingoje shukurani ... songa mbele
  • kuwa na tazamo chanya, ukiwa na mtazamo hasi daima hauwezi kufanikiwa bali jitahidi kuwa na mtazamo chanya ili mambo yako yawe chanya na itakusaidia kuwa jasiri sana

KWANINI NAACHIKA NA KILA MPENZI?

MAPENZI NI NINI? Mapenzi ni hali ya kuwa na ukaribu wa kihisia kingono kati ya mwanamke na mwanaume. Mvutano wa kihisia kati ya jinsia hizo ...