Ujasiri ni nini?
Ujasiri ni hali ya kuamua kufanya jambo gumu linaloweza kuwa si rahisi moyo wako au mtu mwingine kuamua kulifanya bali ukajitoa na kulifanya. mfano mtu unaweza kujitoa hata uhai wako ili hali uokoe watu wengine, ukafirisika hata mali zako ilihali uokoe maskini, ukajitosa mahali poote pale bila woga ili hali upate utakacho.
Ujasiri haupo kwa kila mtu, wapo watu waoga hawawezi hata kujaribu jambo wao hutegemea tu watu wengine ndio maisha yao husonga mbele. Lakini wapo watu ambao hawajali maisha yao wanaweza kufanya lolote hatakama haliwezekani ilimradi waishi maisha mazuri au kupata vitu wavitakavyo kama vile mapenzi, pesa, utajiri n.k
Ujasiri huja wenyewe pale moyo wako unapoamua jambo bilakipingamizi chochote.. hakuna mtu anayefundishwa ujasiri bali huja wenyewe kutokana na msukumo wa moyo au shinikizo la watu fulani au vitu fulani. "woga ni umaskini" ni kauli ambayo watu wanaojiamini na ni majasiri hutumia katika harakati za kimaisha... mfano unakuta mtu anapenda msichana fulani lakini hawezi kabisa hata kumtamkia anaishia tu kuumia sana na kujihisi kama hana bahati.kumbe ndio kukosa ujasiri kwenyewe.
Sababu za kukosa ujasiri- kutojiamini; unakuta mtu anapenda sana vitu fulani au mtu fulani lakini kutokana na yeye kutojiamin anaweza kuvikosa au kumkosa mtu ampendae.......
- kujidharau, kuna baadhi ya watu ujiona wao si mali kitu.. wao wako hadhi ya chini kuliko wengine, au wakajihisi ni wabaya, weusi, waovu sana, hawana akili, maskini kuliko wengine hivyo kujidharau.
- Mitazamo hasi; hii ni mitadhamo iwayo akilini mwa watu ambapo mara nyingi watu hujiona kuwa sahihi kimazamo hasa upinzani wa vitu vyenye tija na kushikilia mitazao isiyo kuwa na tija... mfano kunawatu walisha amini kwamba hawawezi kitu kabisa ndio wakajidharau na kuishia kutojiamini.
- kukosa msaada/support; moyo wa mtu unaweza kukata tamaa na kutojiamini endapo kwa upande wake hakna anae msimamia wala kumtazama hata kama anafanya jambo la msingi badala yake wakajitokeza watu wanao mbeza au kumkejeli hivyo mtu akaona haina maana kuendelea na jambo alilolitarajia na kujikuta amepoteza ujasiri n.k
- kujiamini; hakuna binadamu aliye kamilika, kama umeamua kufanya jambo lolote lenye msaada katika maisha yako au a wengine.. jiamini ujioe hata kama watu watakushangaa, au kukucheka, kukubeza kukukejeli n.k .... "uoga ni umaskini"
- Simama imara mwenyewe; daima usitetereke kwa yale ambayo watu wanakunenea bali simama imara na sikuzote usingoje shukurani ... songa mbele
- kuwa na tazamo chanya, ukiwa na mtazamo hasi daima hauwezi kufanikiwa bali jitahidi kuwa na mtazamo chanya ili mambo yako yawe chanya na itakusaidia kuwa jasiri sana
