Monday, December 11, 2023

KUFAULU KATIKA MAISHA (TO SUCCEEED IN LIFE)

 Mitihani katika maisha ya kila mwanadamu ni jambo ambalo ni la kawaida na ni haki ya kila mmoja wapo anayeishi kwenye huu ulimwengu. Maandiko ya kidini pia hayajamuahidi yeyote kuishi katika raha na starehe bali ni masumbuko mitihani na magumu mpaka siku yake ya mwisho ya kuishi hapa ulimwnguni. 

(Ayu 14:1 SUV

Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke Siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu)

Mateso

Changamoto ni nyingi sana hata ni ngumu kuzieleza zote baadhi tu ni changamoto zinaweza mkumba binadamu yeyote:

1. Magonjwa ya kudumu au magonjwa ya kupita

2. Kufilisika kiuchumi, kupoteza mali zako, kuibiwa n.k

3. Mapenzi na mahusiano

4. Kukosa ajira, kipato

5. Umasikini

6. Kifo, kufiwa

7. Kufukuzwa kazi

8. Majanga ya asili kama vile mafuriko, matetemeko, vimbunga, magonjwa n.k

9. Kudhurumiwa, kutapeliwa, kudanganywa n.k

10. Ajari n.k


kUFAULU KATIKA MAISHA


Zote hizo ni baadhi ya changamoto ambazo mtu unaweza kukumbana nazo muda wowote katika maisha ya kila siku.


NJIA BORA ZA KUEPUKANA AU KUFAULU KUPAMBANA NA MATATIZO HAYA YA KILA SIKU

1. KUMTEGEMEA MUNGU KWA KILA JAMBO✝✝✝

zipo changamoto nyingi sana mabazo kwa uwezo wetu na akili za kawaida hatuwezi kutatua bali MUNGU pekee ndiye anaweza kuzitatua. kama mwanadamu wa kawaida nadhani tunashuhudia mengi ambayo yako nje ya uwezo wetu (beyond human Nature) hivyo hakuna njia ya kupambana nayo bali ni kusimama na imani zetu na Kuomba MUNGU atuepushie kila lililo nje ya uwezo wetu. mfano Magonjwa mfano mzuri Covid 19, majanga ya asili mfano Tsunami tunashudia nchi za Indonesia, Thailand, India, Sri-Lanka, Malaysia, Myanmar, Bangladesh, Maldives, Reunion Island (French), Seychelles, Madagascar, Mauritius, Somalia, Tanzania, Kenya, Oman, South Africa and Australia

Tsunami

💦

2. KUPAMBANA KWA BIDII NA MAARIFA

inakuhitaji Bidii sana na maarifa ili kupambana na changamoto hizo zilizotajwa

  • kwa kufanya kazi bila kuchagua ili mradi tu inakupatia kipato 
  • kutafuta maarifa mapya kila siku yale yanayoweza kukusaidia katika maisha yako ya kila siku.
  • kusali kwa imani yako kila siku 
  • kufanya mazoezi ya mwili kwaajili ya afya bora
  • kuzingatia lishe bora kwa afya yako
  • kubadili mtindo wa maisha mfanyo kuacha/kupunguza uvutaji wa sigara na matumizi ya madawa ya kulevya, kuacha matumizi ya pombe na vilevi, kupunguza idadi ya wanawake/wanaume unaofanya nao mapenzi
  • kufwata sheria zilizowekwa na jamii au serikali yako ili uishi kwa amani
  • Punguza marafiki wale wasiokuwa na msaada kwako


KWANINI NAACHIKA NA KILA MPENZI?

MAPENZI NI NINI? Mapenzi ni hali ya kuwa na ukaribu wa kihisia kingono kati ya mwanamke na mwanaume. Mvutano wa kihisia kati ya jinsia hizo ...