Ugonjwa wa kupooza (stroke) au wengine huita ugonjwa wa kiharusi ni aina ya ugonjwa ambao huathiri mfumo wa fahamu na neva za mwili kiujumla. Ugonjwa huu awali ulikuwa unaweza kuwapata watu wenye umri wa juu au makamo lakini kwa sasa ugonjwa huu unaweza kumpata mtu yeyote yule kuanzia umri wa kati.
Stroke/kiharusi ni ugonjwa mbaya lakini unamatibau yake ambapo mgonjwa anaweza kutibiwa na akapona japo wengine wanapata ulemavu wa viungo na kuathiri ogani za mwili.
AINA ZA STROKE/KUPOOZA
kuna aina Mbili za ugonjwa huu wa kupooza
1. Ischemic stroke
Aina hii ya stroke hutokana na Mishipa ya damu kushindwa kusukuma damu ndani ya mishipa na kusababisha damu kurundikana na kuganda kwenye mishipa iliyopo kwenye Ubongo wa Binadamu. tukio hili hutokea ghafla kama umeme pale ambapo damu au chembe nyekundu za damu zimerundikana sehemu na kufanya mawasiliano ya baadhi ya mishipa kukata hivyo kusababisha kupooza kwa mwili katika sehemu mbalimbali.
Kama tujuavyo kuwa damu katika mwili ndio husafilisha kila kitu katika mwili wa binadamu ikiwemo mawasiliano na umeme wa mwili kupitia veni za mwili. hivyo damu iikwa ghafla imekatwa katika mishipa iliyopo kwenye ubongo inaweza kusababisha mtu kupooza na kupoteza fahamu.- - Kupinda mdomo kwa Mgonjwa
- -Viungo kukakamaa kama vile mikono, shingo au miguu
- - Kusinyaa kwenye ubongo kwa baadhi ya wagonjwa
- - Kupoteza lugha au kuongea
- - Jicho moja au yote kupoteza kuona au kuona kwa uhafifu
- -Kupoteza hisia za miguso au kuguswa na kitu huwawezi kuhisi kitu
- -Kushindwa kutembea au kujongea kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
- -Kupoteza hisia za haja/ kuhisi haja
- -Kutosikia vizuri au kutosikia kabisa
- -Kupoteza kumbukumbu kabisa au kuwa nazo kidogo na mara nyingine kupata ugonjwa wa akili


%202.jpg)