Saturday, December 3, 2022

UGONJWA WA KUPOOZA (STROKE ) AU KIHARUSI

 Ugonjwa wa kupooza (stroke) au wengine huita ugonjwa wa kiharusi ni aina ya ugonjwa ambao huathiri mfumo wa fahamu na neva za mwili kiujumla. Ugonjwa huu awali ulikuwa unaweza kuwapata watu wenye umri wa juu au makamo lakini kwa  sasa ugonjwa huu unaweza kumpata mtu yeyote yule kuanzia umri wa kati. 

Stroke/kiharusi ni ugonjwa mbaya lakini unamatibau yake ambapo mgonjwa anaweza kutibiwa na akapona japo wengine wanapata ulemavu wa viungo na kuathiri ogani za mwili.



AINA ZA STROKE/KUPOOZA

kuna aina Mbili za ugonjwa huu wa kupooza

1. Ischemic stroke

Aina hii ya stroke hutokana na Mishipa ya damu kushindwa kusukuma damu ndani ya mishipa na kusababisha damu kurundikana na kuganda kwenye mishipa iliyopo kwenye Ubongo wa Binadamu. tukio hili hutokea ghafla kama umeme pale ambapo damu au chembe nyekundu za damu zimerundikana sehemu na kufanya mawasiliano ya baadhi ya mishipa kukata hivyo kusababisha kupooza kwa mwili katika sehemu mbalimbali.

Kama tujuavyo kuwa damu katika mwili ndio husafilisha kila kitu katika mwili wa binadamu ikiwemo mawasiliano na umeme wa mwili kupitia veni za mwili. hivyo damu iikwa ghafla imekatwa katika mishipa iliyopo kwenye ubongo inaweza kusababisha mtu kupooza na kupoteza fahamu.

Sababu za Kutokea Kwa Ischemic Stroke.
i. Mafuta kuganda ndani ya Mishipa ya Damu hivyo kufanya njia iwenembaba sana kusukuma damu kwa wakati na kwa usahihi.

ii. Mishipa kuwa miembaba kutokana na lishe duni au uvutaji wa sigara na pombe katika maisha ya kila siku.

iii. Kutofanya Mazoezi na kuwa na unene uliopindukia kupita kiasi

MADHARA YANAYOWEZA KUTOKANA NA UGONJWA WA AINA HII.
  • - Kupinda mdomo kwa Mgonjwa 
  • -Viungo kukakamaa kama vile mikono, shingo au miguu
  • - Kusinyaa kwenye ubongo kwa baadhi ya wagonjwa
  • - Kupoteza lugha au kuongea
  • - Jicho moja au yote kupoteza kuona au kuona kwa uhafifu
  • -Kupoteza hisia za miguso au kuguswa na kitu huwawezi kuhisi kitu
  • -Kushindwa kutembea au kujongea kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
  • -Kupoteza hisia za haja/ kuhisi haja 
  • -Kutosikia vizuri au kutosikia kabisa
  • -Kupoteza kumbukumbu kabisa au kuwa nazo kidogo na mara nyingine kupata ugonjwa wa akili



2. .HEMORRHAGIC STROKE
Aina hii hutokana na Damu kupasua Mishipa ya damu na kuanza kuvuja ndani ya ubongo, mishipa hii midogo sana inayopatikana kwenye ubongo ikianza kuvuja kwenye ubongo inaweza kuganda na kuzuia mawasiliano kwa mgonjwa hivyo kupelekea kupooza.
Aina hii hutokana pale ambapo damu imeshindwa kupita kwenye mishipa ya damu kutokana na msukump mkubwa wa damu hivyo inasababisha mishipa miembaba ndani ya ubongo kupasuka na kumwaga damu kwenye ubongo hivyo kusababisha mtu kupooza


Kwa maelezo zaidi juu ya huu Ugonjwa njoo WhatsApp +255756440628
Nikueleze Tiba na Kinga 
Tiba Vifaa
Tiba Madawa ya asili n.k



No comments:

Post a Comment

KWANINI NAACHIKA NA KILA MPENZI?

MAPENZI NI NINI? Mapenzi ni hali ya kuwa na ukaribu wa kihisia kingono kati ya mwanamke na mwanaume. Mvutano wa kihisia kati ya jinsia hizo ...